KIFO CHA MSANII WA BONGO FLEVA JEBBY CHAZUA UTATA MZITO. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 26 April 2018

KIFO CHA MSANII WA BONGO FLEVA JEBBY CHAZUA UTATA MZITO.

IKiwa zimepita siku chache tokea alipo fariki na kuzikwa msanii wa Bongo Fleva Jebby ambaye alijipatia umaarufu mkubwa enzi za uhai wake na wimbo kama 'swahiba' kumeibuka maswali mengi kwa watu wa karibu huku wakidai kifo chake kimetokana na Imani za kishirikina.

Akizungumza  rafiki wa karibu na marehemu Jebby ambaye pia ndiye aliyekuwa akimuuguza kwa kipindi kirefu wakati alipokuwa Jijini Dar es Salaam Francis Vitus na kusema Jebby kabla ya kufariki alikuwa anauguwa mara kwa mara na idawa alizokuwa amepewa hospitali zilikuwa zikimsaidia kwa kiasi fulani na kurudi katika hali yake.
"Kuna kitu kilikuwa kinanistua cha yeye kutokwa na damu nyingi maeneo ya puani, nilikuwa namuuliza inasababishwa na nini alikuwa anajibu hajui ila anaona zinatoka tu ila kitendo cha damu kukatika anakiona cha kawaida na kufurahi", amesema Vitus.
Pamoja na hayo, Vitus ameendelea kwa kusema "suala la kifo chake kuhusishwa na imani za kishirikina sina imani nalo zaidi ingawa mimi mwenyewe nilikuwa namuuliza lakini alikuwa ananikwepa na kuniambia kama kweli ni vitu vya kishirikina yeye anamuachia Mungu maana kama kufa bora kufa lakini yeye anajiona sawa tu. Ila nilishindwa kuelewa kwa mtu kama yeye nyumbani kwao kwenye msiba kusiwepo na hata turubai nikauliza lakini sikupata jibu". anazidiwa lakini dawa alizokuwa amepewa hospitali zilikuwa zikimsaidia kwa kiasi fulani na kurudi katika hali yake.
"Kuna kitu kilikuwa kinanistua cha yeye kutokwa na damu nyingi maeneo ya puani, nilikuwa namuuliza inasababishwa na nini alikuwa anajibu hajui ila anaona zinatoka tu ila kitendo cha damu kukatika anakiona cha kawaida na kufurahi", amesema Vitus.
Pamoja na hayo, Vitus ameendelea kwa kusema "suala la kifo chake kuhusishwa na imani za kishirikina sina imani nalo zaidi ingawa mimi mwenyewe nilikuwa namuuliza lakini alikuwa ananikwepa na kuniambia kama kweli ni vitu vya kishirikina yeye anamuachia Mungu maana kama kufa bora kufa lakini yeye anajiona sawa tu. Ila nilishindwa kuelewa kwa mtu kama yeye nyumbani kwao kwenye msiba kusiwepo na hata turubai nikauliza lakini sikupata jibu".

No comments:

Post a Comment