MKALI wa Ngoma ya Kaitaba, Said Juma ‘Chegge Chigunda’ amesema miongoni mwa vitu ambavyo hatakuja kuvisahau maishani mwake ni pamoja na msiba wa video vixen, Agnes Gerald ‘Masogange’ uliotokea Ijumaa iliopita.
Chege aliyasema hayo juzi Jumapili alipokuwa Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar katika kuuaga mwili wa Masogange aliyefariki ghafla baada ya kupungukiwa damu.
“Kiukweli msiba umeniumiza kama msanii kwani sisi ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wa mwanzomwanzo kumtoa Masogange kimuziki, kifupi sitamsahau na nawapa pole ndugu na wanafamilia,” alisema Chegge.
Masogange alitarajiwa kuzikwa nyumbani kwao, Mbalizi-Mbeya jana. Atakumbukwa kwa mchango wake katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva akiwa kama video vixen, kati ya video zake zilizokubalika ni pamoja na Msambinungwa ya Tunda Man pamoja na Masogange ya Belle9.
No comments:
Post a Comment