Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema anataka kushinda tuzo saba za Ballon d'Or pamoja na kupata watoto saba.
Ronaldo amefanikiwa kupata mtoto wa 4 wiki hii baada ya mpenzi wake Georgina Rodriquez kujifungua mtoto wa kike ambaye amepewa jina la Alana Martina.
Alana Martina ametanguliwa na kaka zake watatu ambao ni Cristiano Jr pamoja na wengine wawili ambao ni mapacha waliozaliwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Ronaldo mwenye miaka 32 amesema “Nataka kuchukua tuzo za Ballon d’Or mara saba pamoja na kupata watoto saba, nina uhakika hilo litatimia kwasababu nina umri wa miaka 32 na bado najihisi kuwa mwenye nguvu”, amesem Ronaldo.
Hadi sasa Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mara mbili mfululizo akimshinda mpinzani wake Lionel Messi. Ronaldo bado anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or 2017 kutokana na mafanikio ambayo ameyapata msimu uliopita akichukua ubingwa wa La Liga pamoja na UEFA.
No comments:
Post a Comment