SHAMSA FORD ACHARUKA JUU YA MASTAA WA KIKE KUIBIANA MABWANA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 26 April 2018

SHAMSA FORD ACHARUKA JUU YA MASTAA WA KIKE KUIBIANA MABWANA.

MSANII anayefanya vizuri Bongo Muvi, Shamsa Ford amefunguka kuwa hakuna kitu anachokiheshimu kama mwanaume wa mtu wake wa karibu lakini anashangaa wasanii wengi wamekuwa wakiiba wanaume wa watu.

Akizungumza na Amani bila kuwataja majina, Shamsa alisema kuna baadhi ya mastaa wanajua wazi mwanaume anayemtongoza ni wa rafiki yake lakini akijua tu ana fedha yuko radhi hata ajifanye kama hamjui huyo rafiki yake ili mradi tu atembee naye.

“Mimi jamani niko tofauti kabisa siwezi mwanaume wa rafiki yangu akanitongoza nikakubali ninaheshimu hilo lakini wengine wako radhi wakukane ili mradi tu apate fedha,” alisema Shamsa huku akibainisha kuwa hakuna mwanamke atakayemsogelea mumewe Chidi Mapenzi kwani ni mwaminifu na hawezi kumsaliti.

No comments:

Post a Comment