Akizungumza Rammy amesema kulikuwa na kutoelewana kati ya wawili hao huku chanzo kikubwa kikiwa ni kukataa kuwa naye karibu kwa sababu alikuwa na Agness, na kufikia hatua ya kugombana hata sehemu ya kazi wakishoot tamthilia.
“Mimi na Irene Paul hazikuwa zinaenda vizuri tangu muda mrefu, kwa sababu niliona kabisa huyu mtu 'she is on my neck' muda mrefu sana, sijui labda ana interest zake binafsi, kwa sbabu alijaribu hata kujiweka karibu mara kadhaa lakini kwa kweli mimi nilikuwa kwenye mahusiano na Agnes, lakini mwishowe alipodiriki kuniingilia zaidi na kuniambia kwamba unaishi na mtu lakini hujui nani anamlipia kodi zake, nani anamlipia bili zake, wewe unaishi vipi na mtu kama Masogange, unajua Masogange ni msichana expensive, vitu kama hivyo ni dharau kwa mwanaume kumwambia, kwa hiyo mimi nilikasirika naye na niligombana naye mpaka watu wote wa location wa tamthilia walijua”, amesema Rammy Galis.
Rammy Galis ameendelea kwa kuelezea akisema kwamba..."nafikiri huyu mwanamke yupo kwenye situation ya kutokuwa vizuri na mimi muda mrefu akaona hiyo ndio fursa ya kuniongelea mabaya, mimi ni mwanaume ambaye nategemea kazi zangu nategemea utu wangu kutengeneza maisha yangu, sitegemei drama au kiki, kwa sababu sikumbuki kuwepo kwenye drama au kiki”.
Hata hivyo Rammy amesema kwamba hawezi kuendelea kuwa na chuki na Irene Paul kwani alishamsamehe na alishasahau, hivyo hawezi kugombana naye kwakuwa yeye ni mwanaume.
No comments:
Post a Comment