MREMBO VERA SIDIKA AKIRI KUNASA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 1 April 2018

MREMBO VERA SIDIKA AKIRI KUNASA

Mrembo kutokea nchini Kenya ambaye pia ni maarufu kwenye mitandao Vera Sidika amethibitisha tetesi za kuwa ni mjamzito, na kusema kwamba ni kitu ambacho alikuwa anakitamani sana.



Kwenye ukurasa wake wa instagram Vera Sidika ameandika Ujumbe akisema kuwa amejitahidi kuficha suala hilo kwa muda mrefu, lakini ameona ni vyema kuujulisha umma kwani mimba sio jambo la kuweza kuficha muda mrefu bila watu kuweza kukushtukia.

Kwenye post hiyo Vera amesema siku zote alikuwa akitamani kabla hajafikisha miaka 30 awe mama, na anashukuru Mungu kwa baraka alizompa za kuweza kupata ujauzito na hatimaye kusubiria mtoto wake wa kwanza kwa furaha akiwa ndani ya miaka 29 tu.

No comments:

Post a Comment