MOURINHO AZIMA NDOTO ZA GUARDIOLA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 7 April 2018

MOURINHO AZIMA NDOTO ZA GUARDIOLA.

Klabu ya soka ya Manchester United imezima ndoto ya Manchester City na kocha Pep Guardiola kutwaa taji la EPL mapema zaidi kuliko walivo wahi kufanya wao kuchukua ubingwa kabla ya mechi 5 baada ya kuibuka na ushindi ambao ungeamua bingwa.

Katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye uwanja wa Etihad Man United wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji Man City ambao kama wangeshinda leo wangetwaa taji hilo kwa msimu huu wa 2018/19 na kuweka rekodi ya kutwaa mapema zaidi.

Man United ndio inashikilia rekodi ya kutwaa taji la EPL mapema zaidi ikifanya hivyo kabla ya mechi 5 ligi kumalizika ambapo kama Man City leo wangefanikiwa kushinda wangetwaa kabla ya mechi 6 ligi kufika tamati.
Man City walifunga mabao yao mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha Vicent Kompany na kiungo Ilikay Gundogan kabla ya Man United kurejea mchezoni kipindi cha pili kwa mabao mawili ya haraka kutoka kwa Paul Pogba na baadae Smalling kufunga bao la ushindi.

Man City sasa imebaki na alama 84 baada ya mechi 32 huku Man United ikifikisha alama 71 katika nafasi ya pili, ambapo bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa endapo man Cioty atakosa ushindi katika mechi zilizobaki. Mechi ijayo Man City itakuwa ugenini kucheza na Tottenham Hotspur.

No comments:

Post a Comment