KICHUYA APEWA JUKUMU ZITO SIMBA SC - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 7 April 2018

KICHUYA APEWA JUKUMU ZITO SIMBA SC

BAADA ya kufanikiwa kuivuruga Singida United juzi, Mtibwa Sugar wamesisitiza kwamba hizo ni salamu tosha kwa Simba na kuwataka wajiandae kisaikolojia. Lakini kocha kijana wa Simba anayekubalika zaidi na mashabiki, Masoud Djuma amewaambia kwamba majibu yatapatikana uwanjani huku wakimpa majukumu Shiza Kichuya.

Mtibwa yenye pointi 30, inawakaribisha Simba kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ikiwa imeshinda michezo yake miwili mfululizo ule wa FA dhidi ya Azam FC na wa ligi baina ya Singida United timu ambazo zote zinaongozwa na makocha wa kigeni huku wao wakiongozwa na mzawa Zuber Katwila.

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru anasema; “Kwa sasa Mtibwa ipo vizuri ndiyo maana hata Simba hawana raha sababu wameingia na hofu kutokana na kasi yetu ambayo tumeonyesha kwenye michezo miwili ambayo
imepita hivyo hawalali huko wanawaza waje na mbinu gani.”

“Sababu tumeweza kuzifunga timu mbili na zote mabenchi yao ya ufundi yapo na makocha wageni na wachezaji wa kigeni na tunaenda kukutana na Simba nao wakiwa hivyo hivyo. Hatuna kisingizio, tutawapiga.”
Beki wa kati wa Mtibwa, Cassian Ponela ameeleza kuwa; “Sisi kwa upande wetu kama mabeki, tumeshapeana majukumu ya kuhakikisha hao washambuliaji wao tunawazuia ili tufikie malengo.

” Kichuya apewa majukumu Straika mwenye mizuka ndani ya Simba, Shiza Kichuya amekabidhiwa majukumu mazito na kocha mkuu wa timu hiyo, Mfaransa, Pierre Lechantre kuhakikisha anaimaliza Mtibwa.

Lechantre ambaye CV yake ni kubwa kuliko makocha wote nchini, anaamini katika mechi ya kesho washambuliaji wake John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi, watawekewa ulinzi mkali hivyo ni jukumu la wachezaji wake wengine akiwemo, Kichuya kuhakikisha wanafanya mambo.

“Mtibwa Sugar watakuja uwanjani kwa lengo la kuhakikisha Okwi na Bocco hawapati nafasi ya kucheza kabisa lakini wapo wengine kama vile Kichuya nimewapa majukumu ya kufanya pindi hali hiyo itakapojitokeza ili tuweze kupata ushindi,” alisema Lechantre.

No comments:

Post a Comment