MAJIBU 4, WARAKA WA RAY C. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 2 April 2018

MAJIBU 4, WARAKA WA RAY C.

MEI 15, 1982 katika mkoa wa Iringa alizaliwa msanii mkongwe mwenye sauti tamu katika Muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Ray C alianza rasmi muziki huo mwaka 2003, hadi sasa anashikilia albamu nne kwapani ambazo ni Mapenzi Yangu (2003), Na Wewe Milele (2004), Sogea Sogea (2006) na Touch Me (2008).
Q Chief
Ray C ni miongoni mwa wanawake waliosimama kwenye gemu la Bongo Fleva kwa muda mrefu ambapo hadi sasa ameshafanya ziara sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda, Msumbiji, China, Uingereza, Norway, Ujerumani, Uholanzi, Ugiriki, Sweden, Marekani, Australia, Ufilipino, Afrika Kusini, India na Nigeria.
Ray C anashikilia tuzo tatu hadi sasa zikiwemo mbili za Kilimanjaro Tanzani Music Awards (KTMA 2004) na moja ya Kisima (2007) kutoka Uganda.
T.I.D
Hakuna anayebisha kuhusiana na uwezo wake katika kukata nyonga na kutoa sauti awapo jukwaani. Juzikati katika ukurasa wake wa kijamii wa Instagram alikaa na kufikiria mengi kuhusiana na Bongo Fleva ilipo na inapo-tokea.Aliandika ‘waraka’ ambao kimsingi inaonesha dhahiri wanaonufaika na Bongo Fleva ni wachache, katika moja ya mistari yake ameandika;
“Kuna muda huwa nafikiria mambo mengi sana! Huwa najiskia kuamua kutiwa mimba, nizae niwe tu mama wa nyumbani maana nikiangalia wasanii wenye maendeleo kwenye Bongo Fleva ni wachache saaaaana!
“Sijiongelei mimi maana mi mwenyewe kuna wakati nilivurunda! Nakubali nilibugi na nikagundua nimebugi haswa na ndio maana nimepambana mpaka hapa niliko baada ya kugundua baraka tele nilizozawadiwa na Mungu ni kubwa mno kuliko starehe za muda!!!
Banana Zorro
“Ila huwa nakaa najiuliza miaka kama sita ambayo nilipotea kwenye industry! Kuna wasanii nilianza nao na wana vipaji vya ajabu maskini lakini wengi wao wamezimwa kama taa!!! Namkumbuka Nature! Joseline! Bushoke! Z Anto! Matonya! Makamua! Marlow, Domokaya na wengine siwezi maliza!!!!!Wengi sana ni wasanii wakubwa na wana uwezo mkubwa mno! Najiuliza kitu gani kinachowakatisha tamaa hadi leo wamekuwa adimu!!!???”
Baada ya wakaraka huo wa Ray C, Star Showbiz limechimba na kuibuka na baadhi ya majibu juu ya kwa nini wakongwe wengi wamepotea wakiwa na uwezo mkubwa na kitu kinachowakatisha tamaa ya kurudi.
Kutokubadilika Wasanii wengi wa zamani wameshinda kuendana na kasi ya wasanii wa sasa kwa kutokubadilika aina yao ya uimbaji. Wengi wameshindwa kuwika tena kutokana na mazoea ya staili ya kuimba ileile ambayo imezoeleka na mashabiki wengi.
Mr Blue
Wingi wa wasanii wapya Hii inaweza kuwa sababu kubwa ya wasanii wengi kushindwa kurudi kwenye gemu. Zamani wasanii walikuwa wa kuwahesabu na hata studio za kurekodia nazo zilikuwa za kuhesabu.
Zamani msanii ambaye hana lebo mpaka afanikiwe kuingia studio na kuibuka na ngoma lazima apigane hasa, kutokana na hilo sasa, wakongwe wengi wanaotoka kurudi kwenye gemu wakifikiria suala la wingi wa wasanii wengi kila kukicha Kutokujiamini
Wengi wao wamekuwa na hofu kuwa wasanii waliopo wanaweza kuwapoteza endapo watatoboa tena. Kuna waliojaribu kutoa ngoma mbili baada ya kufeli sokoni wakaamua kuachana na muziki kabisa.

Matabaka
Bongo Fleva ya sasa ipo tofauti sana na zamani. Ukizungumzia matabaka kwa kipindi cha nyuma yalikuwa kwenye makundi tu, mfano wa makundi yaliokuwa yakishindana na kukubalika na wengi ni Gangwe Mobb, Daz Nundaz, Wagosi wa Kaya, East Coast Team (ECT), Solid Ground Family, Manzese Crew, Hard Blasterz Crew (HBC) na mengine kibao.
Licha ya makundi hayo kutengeneza matabaka kwenye muziki, bado kuna wasanii walikuwa wakitoka kwenye makundi hayohayo na wengine bila makundi na walikuwa wakikubalika mfano, Sugu (2Proud), Balozi Dola Soul, Q Chief, TID, Banana Zorro, Dully, Mr Blue na Fid Q.
Kwa sasa matabaka yamekuwa siyo kwenye makundi bali kwa wanamuziki mmojammoja, mfano kuna wasanii wachache wanaokubalika sana (Diamond na Alikiba) ambao wametengeneza mashabiki wao damdam, kuna wale saizi ya kati (Ben Pol, Billnass, Maua Sama, Linah, Barnaba na Mo Music pia kuna ambao wa chini kabisa (underground).

No comments:

Post a Comment