STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Kajala Masanja ametoa kali baada ya kusema kuwa katika vitu ambavyo havipendi ni kulala na nguo usiku japokuwa bado hajaolewa.
Akizungumza Kajala alisema kuwa, jambo la kwanza ambalo mtu akimwingilia usiku wa manane, atakiona ni mwili wake maana kuvaa nguo yeye usiku ni mwiko hata kuwe na baridi kiasi gani analala hivyohivyo.
“Jamani ukiniambia nivae nguo usiku, unaweza kunichapa fimbo maana siwezi hata kidogo yaani siku mtu akiniingilia usiku kuniibia, anaweza kuachana na zoezi hilo akaanza kunikodolea macho,” alisema Kajala huku akicheka.
No comments:
Post a Comment