Aunty Ezekiel amesema kuwa nguo wanayosema ameazima zilishonwa mbli na yeye ndiye aliyekuwa wakwanza kuvaa nguo hiyo lakini anashangaa sana watu wanapokuja na kumtuhumu kuhusu swala hilo.
Hata hivyo Aunty anasema kuwa bado kwao sio shida kuvaliana nguo kwa sababu ni marafiki hivyo ni swala la kawaida.
"Kwanza kuazima nguo sio shida kwetu kwa sababu ni rafiki yangu lakini cha ajabu ni kwamba nguo wanayoizungumzia wao zimefanana wala hakuna aliyenda kugonga hodi kwa mwenzake."-Alijibu Aunty
Wawili hao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa ingawa hapo katikati walikuwa wakionekana kutokuwa pamoja lakini sasa ivi mapenzi yamerudi na kuwa mapya kabisa.
No comments:
Post a Comment