Muimbaji huyo wa WCB ameiambia Funiko, Radio Five kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa kuwa ana sababu zake za msingi.
“Mimi na heshimu sana maamuzi ya mtu, siwezi kuzungumza kama ni vibaya au ni vizuri, kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu mahusiano ndio sina,” amesema.
Alipoulizwa iwapo kipindi wawili hao walikuwa katika mahusiano kuna baadhi ya vitu alinufaika navyo kutoka kwa Zari, Harmonize alijibu;
“Kuzungumza amenisaidia au hajanisaidi sio kitu kizuri halafu kwa njia moja au nyingine unaweza kuonekana ni mnafiki, kwanini usiseme siku zote uje useme leo,” alieleza.
Mnano February 14 mwaka huu katika siku ya wapenda nao Zari The Boss Lady ambaye ni mzazi mwenzie na Diamond Platnumz, aliposti Ua Jeusi katika mtandao wa Instagram na kutangaza kuachana kimahusiano na msanii huyo rasmi.
No comments:
Post a Comment