Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa Klabu hiyo, Jaffar Idd wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo wao dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili (Aprili 8, 2018) katika dimba la Sokoine.
"Tunakwenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunacheza na kupata pointi tatu muhimu ili tuzidi kuimarika katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Sisi kama Azam FC tumeanza mazoezi tokea siku ya Jumatatu kwa ajili ya kujiweka sawa katika mchezo huo, tunajua utakuwa mchezo wenye ushindani na mgumu lakini tutahakikisha tunafanya vizuri", amesema Jaffar.
Kwa upande mwingine, timu ya Azam FC wanatarajia kuondoka leo (Ijumaa) kuelekea mkoani Mbeya tayari kwa mchezo huo
No comments:
Post a Comment