"DOGO JANJA NI MIONGONI MWA WANAFIKI" : EDU BOY. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 20 April 2018

"DOGO JANJA NI MIONGONI MWA WANAFIKI" : EDU BOY.

Msanii wa Hip Hop anaye wakilisha jiji la Mwanza, Edu Boy amefunguka na kumchana Dogo Janja kuwa katika wasanii aliosema ni wanafiki naye ni miongoni mwao kwa sababu ameshindwa kuweka wazi jambo watu alio kuwa amekaa nao kuzungumza sakata la Nandy la kusambaa video za utupu mitandaoni.

Edu Boy ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja ku-post katika ukurasa wake wa kijamii kuwa anasikitishwa na tabia ya baadhi ya wasanii kupenda kuwaona wenzao wanapatwa na majanga ili waporomoke kisanaa.
"Mtu kama Dogo Janja sio kama alikuwa hajui, alikuwa anafahamu vizuri sana sema ule ujasiri wa yeye kuamua na kusema ni kweli wasanii wengi tunaishi kinafiki ndio alikuwa hana. Ila vilevile katika watu wanaoishi kinafiki naye yumo ndani yao kwasababu aliongelea suala la Nandy halafu akashindwa kuwaweka wazi hao watu alikuwa amekaa nao kuzungumzia jambo hilo", amesema Edu Boy.

No comments:

Post a Comment