DADA wa mwanamuziki Ali Salehe Kiba, Zabibu Kiba ameibuka na kueleza alivyoanzisha uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa Timu ya Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda.
Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni, Zabibu alifunguka mambo mengi kuhusiana na penzi lao na yafuatayo ndiyo mahojiano yenyewe:
Risasi Jumamosi: Zabibu,Banda amekutaja kama mpenzi wake, je unaweza kuelezea ni wapi mlikutana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi?
Zabibu: Hapana, yeye ndiye aliyenitafuta mimi, sasa sijui aliniona wapi au nani alimuunganishia.
Risasi Jumamosi: Mbona huweki wazi? Hata kama alikutafuta si kuna sehemu mlikutana? Funguka tu.
Zabibu: Yeye Banda alinipigia simu mimi ndiy maana nikasema alinitafuta.
Risasi Jumamosi: Kuna makala ilitoka kwenye gazeti la Championi ambapo Banda alikutaja kuwa wewe ni mpenzi wake, ulijisikiaje maana wewe hujawahi kuliweka hilo wazi kwenye vyombo vya habari.
Zabibu: Mh! Kama alinitaja sawa ila suala la ndoa siwezi kuliongelea kwa sababu bado Banda hajaja nyumbani kutoa posa.
Risasi Jumamosi: Kwa sababu kaweka wazi uhusiano,bila shaka ndoa ipo karibu ujipange tu. Au wewe hutaki
ndoa unataka mapenzi tu? Zabibu: Nasisitiza kwamba,iwapo atakuja nyumbani ndio nitajua kuwa natarajia kuwa mke wa mtu lakini kwa sasa siwezi kuliongelea hilo.
Risasi Jumamosi: Wanawake wengi wanapenda sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wachezaji maarufu, umejizatiti vipi kwa wale ‘nyakunyaku’?
Zabibu: Unajua wazi kuwa hilo huwezi kulikwepa, cha muhimu ni kuamini kuwa mtu uliyenaye anakupenda na anakuheshimu basi.
Risasi Jumamosi: Mko kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda gani sasa?
Zabibu: Kwa muda wa miaka minne sasa, hivyo tunajuana vizuri tu. Siyo kwamba hatukutani na vikwazo, tunakutana navyo lakini tunakaa chini tunamaliza tofauti zetu kisha tunaendelea.
Risasi Jumamosi:Nakushukuru sana na nakutakia kila la heri.
No comments:
Post a Comment