YANGA WAKICHUKULIA POA WATAONDOKA TENA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 23 March 2018

YANGA WAKICHUKULIA POA WATAONDOKA TENA.

POLE sana kwa Simba ambao kwa sasa wame­baki na Ligi Kuu ya Tanza­nia Bara tu likiwa ndiyo kombe wanaloweza kulichukua msimu huu pamoja na kwamba mwan­zoni mwa msimu walikuwa wa­nawania makombe matatu.

Kwa wengi mwanzoni kama ungewaeleza kuwa mwisho wa Simba msimu huu ungekuwa hivi wasingekuelewa kutokana na hali ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu.

Gumzo kubwa kwa Simba mwanzoni mwa msimu huu ilikuwa usajili wake, wengi waliamini kuwa timu hiyo itatikisa soka la Tanzania.

Kila kukicha majina makubwa yalikuwa yanasajiliwa na timu hiyo, lakini mwisho inaonyesha kuwa timu nyingine nazo zilikuwa zinafanya maandalizi yake.

Hata hivyo timu nyingine ikiwemo Yanga bado zinapam­bana kwenye makombe mengi, Yanga wapo kwenye FA, Ligi Kuu Tanzania Bara na ndiyo timu pekee ya Tanzania ambao ipo kwenye Kombe la Shirikisho Af­rika.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba Yanga wamepangwa na timu ya Ethiopia Wolaitta Dicha ambayo ni timu changa kabisa kwenye michuano ya kimataifa.

Timu hii haijawahi kushiriki mi­chuano ya kimataifa huko nyuma, hii ni ndiyo mara yake ya kwanza na tayari imeshafanya mambo makubwa ya kuitangaza.

Katika hatua iliyopita timu hiyo iliweza kuwatupa nje Zamalek ya nchini Misri, nafikiri kwa wapenda soka watakuwa wanafahamu kila mtu atakaposema kuwa imewatoa Zamalek.

Hii ni timu kubwa kwa Bara la Af­rika na ukitaja miamba mitano ya soka la Afrika huwezi kuacha ku­wataja hawa.
Kama utakuwa na rekodi kuwa Simba waliwahi kuitoa Zamalek kwenye michuano mikubwa pale nchini kwao Misri basi elewa pia kuwa hawa nao wamewaondolea pale pale kwao, hivyo siyo timu ya kubeza.

Nchini kwao inatajwa kama timu changa lakini ambayo inakuwa kwa kasi kubwa sana, inatajwa kama timu ambayo haina safu nzuri sana ya ulinzi lakini ikiwa na washambuliaji matata sana na ambao hawakati tamaa jambo am­balo limeweza kuwapa mafanikio makubwa sana.

Tatizo kubwa sana kwa soka letu imekuwa dharau, Yanga wanataki­wa kuichukulia timu hii kama timu kubwa Afrika na kuacha kuiona kama vile haiwezi kufanya jambo lolote kwa kuwa yenyewe im­eanzishwa mwaka 2009 na Yanga mwaka 1935, hii siyo sawa hata kidogo.

Umri wa timu haikupi nafasi ya kudharau, ukweli ni kwamba Yan­ga wanatakiwa kuona kama vile wamepangwa na Enyimba, lakini wapambane kwanza kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza hapa nyum­bani.

Ushindi wa Yanga hapa nyum­bani utawapa nafasi kubwa zaidi ya kwenda ugenini na kitu mkono­ni, lakini kama Yanga watakubali kuchapwa hapa wakiwa wanafikiri watakwenda kushinda ugenini, huu utakuwa uongo.

Yanga hawana siku nyingi sana za maandalizi hivyo ni vyema basi wakaanza kujiandaa sasa, kama ni kutaka kumfahamu mpinzani wake basi ni sasa badala ya kusubiri dakika za mwisho ndiyo waanze kuwachunguza.
Hii inaweza kuwa nafasi kubwa sana ya Yanga kufuzu makundi ya michuano hiyo kama wataweka dharau mbali na kujiandaa kwa nguvu kubwa kwenye michuano hii.

No comments:

Post a Comment