MWANAMITINDO wa Bongo, Agness Mmassy ameibuka na kueleza jinsi anavyodatishwa na mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mbasha na ndiyo maana amekuwa akiweka picha zake kwenye kurasa zake zote za mitandao ya kijamii kwani anashindwa kujizuia.
Habari za awali zinadai kwamba, wawili hao kwa sasa ni wapenzi na wamekuwa wakijiachia kimahaba sehemu tofauti, lakini Za Motomoto News ilipomtaiti Agness alifunguka kuwa, kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia jambo hilo ila Mbasha ni mwanaume ambaye anampenda hadi anashindwa kujizuia wala hawezi kuficha kwa sababu kumpenda mtu siyo dhambi.
Agness alisema kuwa, kwa jinsi anavyompenda Mbasha, hawezi kujificha hata mwimbaji huyo anajua kwamba anampenda na kwa sasa yupo kwenye harakati za kubadilika ambapo ataokoka ili aweze kuendana naye. “Ninampenda sana Mbasha, naye anajua, kuhusu kujiachia naye ni mapema sana kuzungumzia kwa sasa, muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi, maisha yanabadilika na hivi karibuni tu nitaokoka ili niendane na Mbasha,” alisema Agness anayesifika kwa kutupia picha za nusu utupu kwenye mitandao ya kijamii.
Alipo tafutwa Mbasha na kuulizwa kuhusu kuzimikiwa na mrembo huyo na kwamba ana uhusiano naye, alisema hamfahamu na kama ni kupendwa anapendwa na wengi hivyo haoni ajabu.
TOA MAONI YAKO HAPA
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment