NAFASI NYINGINE YA TAIFASTARS KUONYESHA MAUJUZI YAO LEO - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 1 September 2017

NAFASI NYINGINE YA TAIFASTARS KUONYESHA MAUJUZI YAO LEO

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Botswana, leo Jumamosi zinapambana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ni wa kufuata Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Timu zote zinautumia mchezo huo kama maandalizi ya mechi zao za kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Katika mchezo huo, mwamuzi wa kati anatarajiwa kuwa Elly Sasii akisaidiwa na Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, alisema: “Kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo huu ambao kwetu
ni muhimu kwa maana mbili, moja ni kujiandaa na michezo ijayo ya kufuzu Afcon, lakini pili ni kutafuta nafasi ya kupanda kwenye viwango vya Fifa.
“Kikubwa Watanzania wajitokeze uwanjani kutusapoti kwani vijana wamenihakikishia kwamba wana uwezo wa kushinda mchezo huu.”
Kwa upande wake Kocha wa Botswana, Major David Bright, alisema: “Tumekuja lakini bado tuna uchovu wa safari, lakini tunatarajia kuwa na mchezo mzuri dhidi ya Tanzania kwani hii si mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana.
“Nimepewa kikosi hiki hivi karibuni, lakini nimejaribu kuchukua wachezaji wale wazoefu na naamini tutafanya vizuri. Mechi hii ni kipimo kwetu kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu Afcon.”

1 comment:

  1. Mimi ni blogger lakini pia nafanya kazi ya kutengeneza na kudesign website, blogs Apps na mengineyo. Kama unahitaji App kwa ajili ya blog yako nicheki kwa 0744525792 au email. ombeniutembele@gmail.com. Hizi hapa ni baadhi ya kazi zangu www.laelayetublog.com wwww.fursaajira.com www.nuruafrika.org https://mbaostudio.blogspot.com na nyinginezo

    ReplyDelete