MSAMI KUVUNJA NDOA YA DOGO JANJA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 29 March 2018

MSAMI KUVUNJA NDOA YA DOGO JANJA.

Mwanamuziki anaye Fanya vizuri na ngoma ya 'Mdundo' Msami Baby amesema haoni tatizo lolote la yeye kumsifia mke wa Dogo Janga (Irene Uwoya) kwa madai kuwa wana historia ndefu ya maisha yao hata kabla ya kuolewa hivyo hatitakuwa rahisi kuacha kumsifia.

Msami ameeleza  baada ya wawili hao kuzua ngumzo mitandaoni kwa kile kilichoonekana kuwa bado wanatamania kimapenzi japokuwa mmoja wapo amekuwa mke wa mtu kwa sasa.
"Ni kweli Uwoya anapenda ninayokifanya ndio maana ameni-post ni kweli kwani kuna kitu gani cha uongo hapo wakati amezungumza ukweli. Kama kucheza ninacheza kwa hiyo anahaki ya kusema anachotaka. Na mimi kuandika mtu fulani ni mzuri sio dhambi kwasababu kwangu mimi binafsi naona kama upendo wa kumkubali mtu kama yeye alivyoona kuwa mimi ninasifa ya kuwa mchezaji bora",amesema Msami
Pamoja na hayo, Msami ameendelea kwa kusema "mimi namjua Uwoya tokea zamani, kwa hiyo tuna maisha yetu na historia, tunaongea na kutaniana mambo mengi,'so' haviwezi vitu kama hivyo kuanza kupotea tu". 

No comments:

Post a Comment