Chirwa,Tambwe wakazi gani bwana - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 9 January 2018

Chirwa,Tambwe wakazi gani bwana

KAMA ulikuwa unadhani Yanga kwa kutinga kwao nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi ingekiongezea nguvu kikosi chake kwa kuwaleta Obrey Chirwa na Amissi Tambwe, basi pole yako.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara wamesema wachezaji waliopo sasa visiwani hapa ndio watakao liamsha mpaka mwisho wa mashindano hayo yaliyo asisiwa mwaka 2007.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema nikweli awali walikuwa na presha kubwa kwa kukosekana kwa nyota wake wa kikosi chakwanza, wakiwamo Chirwa, Tambwe na wengine wenye matatizo tofauti, lakini presha hiyo imepungua.

Nsajigwa alisema kukosekana kwa Chirwa na Tambwe katika kikosi chao walasi shida kwa vile waliopo wametosha kabisa kufanya kazi ambayo wanahitaji kuiona kutoka kwao.

“Nimekuwa nikiulizwa sana hili swali, lakini niseme wazi waliosalia wameifikisha timu hii hapailipo, hivyo ndiowatakaomalizamechi zilizosalia, wameonyesha uwezo,” alisema Nsajigwa.

“Hatutawaongeza Chirwa na Tambwe, sidhani kama linaweza kutokea, kwani Yanga ina wachezaji wengi waliofanya kazi nzuri mpaka hapatulipofika.

“Unajua hata tulipofanya usajili tuliangalia uwezowa kila mmoja wa namna anavyoweza kuisaidia Yanga kufanya vizuri, ndio maana na sema waliopo watafanya kazi.”

No comments:

Post a Comment