Kauli ya kingunge yaibua wapinzani - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 7 January 2018

Kauli ya kingunge yaibua wapinzani

 Viongozi wa vyama vya upinzani wamesema kauli ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru kwamba CCM ni chama chake, nimaoni yake binafsi na hayaondoi ukweli kuwaameshiriki kukijenga chama hicho tawala.

Akizungumza na Rais John Magufuli aliyemtembelea hospitalini juzi, Kingunge alisema:“CCM nichama changu, nimetoka tu, nimeachana. Lakini nimefanya kazi zote. Nimejipinda mimi kweli kweli. Kwa hiyo hakiwezi kuwakinyume changuhatakidogo.”
Kauli hiyo ilitafsiriwa na Rais Magufuli kuwa Kingunge bado niCCM moyoni, lakini wapinzani waliohojiwa nao wana maoni yao.

“Hiyo huwa haibadiliki. Ukiasisi chama na ukiachana nacho, utaendeleakuwa muasisi wake,” alisema mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ambaye pia semakauli ya mwanasiasa huyo mkongwe pia ililenga kumkumbusha Rais kwamba pamojana yote yaliyotokea, Kingunge ataendelea kuwa muasisi wa CCM.
“Nadhani hicho ndicho alicho kilenga Kingunge. Ni kamaalikuwa anamkumbushaRais,” alisemaMtatiro.
Kingunge aliyetengaza kuhama CCM Oktoba 4, 2015 alitoa kauli hiyo juzi akiwakitandani Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako anatibiwa majeraha ya kung’atwa nambwa takribani siku sita zilizopita.

Katika maelezo yake, Mtatiro alisema Kingunge ana haki ya kutoa maoni na kwamba huo ndio ukweli.

“Tangu kuanzishwa kwa TANUwao ndiyo waliokipigania na kuunda CCM na ndiyo wazee ambao wamekifikisha kilechama kilipoleo. Waliopo sasa wamekikuta nakuendeleza walipoishia wao,” alisema Mtatiro.

“Kauli yake inamaanisha kuwa hata akipata matatizo, wana-CCM hawataweza kumkimbia pamojana kwamba alijitoa.”

Alisema japo kuwa mwanasiasa huyo hakuwahi kusema amejiungana chama gani, aliondoka CCM vizurina aliweka wazi sababuza kukikimbia chama hicho.

Nayekatibumkuu wa NLD, Tozi Matwange alisema kauliya Kingunge haumaanishi kuwa anaweza kurejea.

Alisema kauli ya mwana siasa huyo inaonyeshadhahiri kwamba CCM ni chama chake kwani alishiriki kukiasisi, kukisimamia.

“Ametoka huko na hatabadilika,” alisema.
Katibumkuu wa NCCR– Mageuzi, Danda Juju alisemaKingunge amefanya kazi kubwaakiwa ndani ya CCM katika kipindi chote chamaisha yake, hivyo kaulihiyo anatafsiri kuwa kumbukumbu zake bado zipo katika chama hicho japokuwa amekiacha.

Wakatihuohuo, mtoto wa mwana siasa huyo, Kinje Mwiru amezungumza kuwa juzi mchana walimpataarifa Kingunge kuhusukifo cha mkewe, Pares najana akaridhia azikwe Alhamisi.

Pares alifariki dunia Januari 4saa 8:00 mchanaakiwa wodiya Sewahaji alikokuwa amelazwa, tangu Oktoba 3 mwaka jana.

“Mzee ametupamwongozo wa nini chakufanya. Mazishi yatafanyika Alhamisikatika makaburi ya Kinondoni,” alisema.

“Mpaka sasa ratiba bado haijapangwanaleo jioni (jana) familia itakutana na kutakuwa nakikao pale nyumbani,” alisema.

No comments:

Post a Comment