SITOKAA NA KUGOMBANA NA EX WA MOSE IYOBO. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 24 March 2018

SITOKAA NA KUGOMBANA NA EX WA MOSE IYOBO.

Msanii wa Filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye pia ni mpenzi wa Mose Iyobo amesema alikuja kugundua kugombana na mpenzi wa zamani wa Iyobo ‘Mwengi’ ni kitu ambacho hakina maana yoyote.

Muigizaji huyo amesema hata wangeendelea kugombana kusingebadilisha majina ya watoto wao ambao wamezaa na Iyobo na si kitu kizuri kwa watoto hapo baadae.

“Katika vitu ambavyo vilipita nilishaandika nikasema sitakaa nigombane na Mwengi tena kwa sababu nimekuja kugundua ni ujinga mwisho wa siku hata nigombane naye miaka mia yule mtoto wake hawezi kuja kubadilika jina,” amesema na kuongeza.

“Lazima mwisho wa siku ataitwa fulani fulani Iyobo, hivyo hivyo kwa Cookie, kwa hiyo wale tayari ni ndugu halafu sasa hivi mitandao ni mengi baadae wakija kuone mama yangu na huyu walikuwa wanagombana itakuja kuwaletea shida watoto,” Aunt Ezekiel ameiambia Bongo5.

Kwa sasa Aunt Ezekiel yupo mbioni kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Mama, katika filamu hii amecheza na mwanae, Cookie.

No comments:

Post a Comment