Skendo ya kufuga mateja yazidi kumtafuna Jike Shupa.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 27 February 2018

Skendo ya kufuga mateja yazidi kumtafuna Jike Shupa..

BAADA ya hivi karibuni kufunguka kuwa, anamsaidia mdogo wa Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Amos Bulaya, Deus Bulaya aliyeathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, muuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amekumbwa na skendo nzito kwamba anafuga mateja (watumiaji wa unga) nyumbani kwake.

Habari zilizoifikia Za Motomoto News, ni kwamba Jike Shupa ambaye anaishi maeneo ya Mwananyamala Hospitali, Dar amekuwa akiwafuga vijana kibao walioathirika kwa unga ambao wanapatikana kwa wingi eneo hilo huku akiishi nao nyumbani kwake bila utaratibu.

“Jike Shupa anawafuga mateja wengi sana maana ana chumba maalum kabisa kwa ajili yao na wengi ni wale wanaotumia dawa kwa ajili ya kuacha unga (methadone). Watu wanadai kwamba kuna vitu anafaidika navyo kwani watu kama hao wakati mwingine wanapora na kumletea yeye kama mama yao,” alisema Hassan, jirani wa Jike Shupa.

Za Motomoto News ilizungumza na Jike Shupa kuhusu tuhuma hizo ambapo alisema ni kweli alikuwa akiwasaidia vijana wengi ambao walikuwa wanatumia methadone, lakini kwa sasa wamesharudi makwao.

“Si kweli kwamba wanapora, nilikuwa ninawasaidia, lakini wameshamaliza muda wao wa kunywa dawa wamerudi makwao,” alisema Jike Shupa.

No comments:

Post a Comment