Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Yahya Msulwa amefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Gratian Mkoba ameithibitisha Mwananchi leo Ijumaa Novemba 17 wakati akizungumza kwa simu.
Mkoba amesema, “Ni kweli amefariki jana usiku na alipelekwa jana hiyo usiku kwa mujibu wa ndugu zake walionipa taarifa, maana mimi nilikuwa nina wiki moja hatujawasiliana na sijui alikuwa na anasumbuliwa na nini,”amesema Mkoba.
Amesema hivi sasa yupo njiani kwenda nyumbani kwa marehemu Tuangoma kujua taratibu za mazishi.
No comments:
Post a Comment