Mapenzi moto moto Gigy money na mpenzi wake wamalizana tofauti yao.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 14 February 2018

Mapenzi moto moto Gigy money na mpenzi wake wamalizana tofauti yao..

MWANADADA ambaye ni mwana-muziki na muuza sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, hivi karibuni amefunguka kwamba, hana matatizo tena na baba wa mtoto wake mtarajiwa aitwaye Mo Jay, na kwamba kila kitu kwa sasa wamekwisha kiweka sawa ambacho kilikuwa kinawafanya wagombane mara kwa mara.

Akizungumza  Gigy aliongeza kuwa, wawapo wawili ‘tafaruku’ ndogondogo huwa hazikosekani, jambo ambalo lilikuwa linajitokeza kwao, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa na hawana tatizo kabisa.

“Sina shida yoyote na mpenzi wangu kwa sasa, kila kitu kipo sawa na yakiwepo ya kuzun-gumza kama tuna matatizo nitazu-ngumza huko mbele, lakini kwa sasa hakuna tatizo lolote,” alisema Gigy. 

No comments:

Post a Comment