Amber Lulu aoga mvua ya matusi.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 14 February 2018

Amber Lulu aoga mvua ya matusi..

MUUZA nyago machachari kwenye video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’, ambaye sasa amegeukia kwenye muziki wa Bongo Fleva, amejikuta akioga mvua ya matusi baada ya kuweka picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram iliyomuonesha maungo yake ya siri.

Akizungumzia sakata hilo, Lulu alisema kuwa anawashangaa watu waliokurupuka kumtolea matusi hayo wakati yeye aliweka kwa kujifurahisha na kwamba hakuona tatizo kwani ni nguo ya kawaida japo inaangaza sana.

“Kwani pale tatizo ni nini? Watu wakiona nguo imekubana kidogo na inaonesha mambo basi ndiyo wanakushambuliaaa,” alisema Amber.

No comments:

Post a Comment