CCM yaibuka kidedea matokeo ya ubunge.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 17 February 2018

CCM yaibuka kidedea matokeo ya ubunge..

Kilimanjaro. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Tume ya Uchaguzi (Nec), kumtangaza Dk Godwin Mollel kuwa mshindi wa kiti hicho.

Nec imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake,  Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.

Kwa upande wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, hadi saa saba usiku shughuli ya majumuisho ya kura ilikuwa inaendelea lakini matokeo ya awali yaliyobandikwa na wasimamizi wasaidizi katika vituo mbalimbali vya kupigia kura, yanaonyesha kuwa mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anaendelea kuongoza.

Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu pamoja na mgombea wa Cuf, Rajab Juma akifuatia kwa tofauti ya kura nyingi.

No comments:

Post a Comment