Tambwe arudishwa Dar - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 8 January 2018

Tambwe arudishwa Dar

Mshambuliaji wa Yanga, Amiss Tambwe amelazimika kurejeshwa Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na Maralia.

Tambwe alikuwa Zanzibar na timu yake inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga,Edward Bavu alisema wamelazimika kumuondoka mchezaji huyo kambini na kurejea Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

"Ana malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu hivyo tumelazimika kumrejesha Dar es Salaam ili apate matibabu zaidi"alisema Bavu.

Katika mashindano hayo ya Mapinduzi ambayo Yanga imefuzu hatua ya nusu fainali,Tambwe hajacheza hata mchezo mmoja.

Mchezaji huyo alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu aumie katika maandalizi ya msimu huu wa Ligi Kuu Bara, lakini akaja kurejea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho(FA) dhidi ya Reha FC na kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 ilioupata Yanga siku hiyo.

No comments:

Post a Comment