Kwasi awapiga mkwara Chirwa na Ajibu - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 8 January 2018

Kwasi awapiga mkwara Chirwa na Ajibu

 Baadaya kufunga bao katikamchezo wake wa kwanza, beki wa Simba, Asante Kwasi amefunguka kwa mara ya kwanzakuhusu ubora wa washambuliaji Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu wa Yanga.

Kwasi amejiunga naSimba kutoka Lipuli yaIringa katika usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Novemba 15 hadi Desemba15, mwakajana.

Haikuwa kazirahisi kwa Lipuli kumpa ruksa ya kuondokabeki huyo wa kati kutokana na ubora naumuhimu wake katikakikosi hicho.

Lakini, juhudi za vigogo wa Simbakuishawishi Lipuli zilizaa matundana mchezaji huyo wa kigenikutoka Ghanani maliya Wekundu wa Msimbazi.

Kwasi amedhihirishaubora wake na Simbabaada ya kufunga bao katikamchezo wake wa kwanza dhidi ya Jamhuri katikamashindano ya Kombe la Mapinduzi.Simba ilishindamabao 3-1.

Muda mfupi baada ya kupata mafanikio hayo, beki huyo amewageukiaChirwa naAjibu akitamba kuwa atawanyoosha.

Akizungumza mjini hapa, Kwasi alidai kuwa Chirwa naAjibu ni washambuliaji hodari wasumbufu, lakinidawa yao inachemka.

Kwasi alisema Chirwa mwenye mabaosita naAjibu matano ni wachezajini hatari wanapokuwa langoni mwa adui kwa kuwa wana kipaji cha kufunga.

 “Chirwa naAjibu nimekutana nao katika Ligi Kuu, nilicheza vizuri dhidi yao lakinikama tutakutana tena nitawapa ulinzi mkali,” alisema Kwasi.

Yanga ina mabao17 yakufunga katikamashindano yaLigi Kuu naChirwa, Ajibu hao wamefunga jumla yamabao 11 namengine sitayakifungwa na wachezajiwengine.

Kwasi aliye anza kutamba akiwa Mbao kabla yakutimkia Lipuli, alisema anaonafahari kuitumikia Simbakwa kuwa ni klabu kubwa nchini.

“Simba nafahamu wana kiu kubwa ya kuchukua ubingwaa wa Ligi Kuu Tanzania Bara nina imani kwa kushirikiana na wenzangu tushinda,”alisema Kwasi.

Katika hatua nyingine, Kwasi juzi alimwaga chozi baada ya mechi yao dhidi yaAzam FC kumalizika kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Idd Kipagwile.
Timu hiyo leo inateremka uwanjani kuwania pointi tatu muhimu dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A.

No comments:

Post a Comment