Lava lava: kuvaa misalaba haina noma. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 14 January 2018

Lava lava: kuvaa misalaba haina noma.

Mwaka jana kulikuwa na stori nyingi mtandaoni kuhusu Wasanii wa WCB kuvaa mikufu yenye misalaba shingoni kitu ambacho baadhi ya watu wame kuwa wakihusisha naimani tofauti tofauti huku baadhi ya waislamu wakidai kuwa hiyo ni ishara ya kukubaliana na dini ya Kikristo.

Sasa msanii wa Bongo Fleva kutoka WCB, Lava Lavalava amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu hiyo ya kuvaa cheni hizo zenye misalaba akidai kuwa ni Swaga tu hakuna jambo lingine nyuma ya misalaba hiyo huku akika na kuwa ile siyo misalaba kama inayotumiwa na Wakristo makanisani.

“Mimi sijawahai kuona msalaba ambao una duara kwa juu, sijawahi kuona, ama msalaba huwa unakuwa hivyo?, mimi sijui labda kama kuna mkristo atusaidie alama ya msalaba huwa inakuwa vipi?“amesema LavaLava mnakuelezea sababu ya WCB kuvaa cheni zenye misalaba,”Mimi sijavaa msalaba ile mimi naona ni swaga tu, yaani ni swaga tu hakuna ishu“.

Tukio la Wasanii waWCB akiwemo kiongoziwaoDiamond Platnumzla kuvaa cheni zenyemisalaba mwishoni mwa mwakajana (2017) liliibua hisia tofauti tofautikwawauminiwadini ya Kiislamu wakiwepo mashekhe waliokuwa wanahoji kuwa muislamu halisi hawezikuvaa msalaba wala kutamka neno ‘Hallelujah’ kama Diamond alivyofanyakwenyewimbo wake wa Hallelujah.

No comments:

Post a Comment