Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirikisho la soka nchini TFF pamoja na lile la Kimataifa FIFA, itajenga kituo cha kisasa cha michezo Mkoani Tanga.
Hilo limebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza, jioni hii wakati akizundua mashindano ya Kombe la Aweso Wilayani Pangani mkoani Tanga.
"Serikali kwa kushirikiana na TFF na FIFA iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo Jijini Tanga, na hizo ndio jitihada za kuboresha michezo nchini kwani kupitia kituo hicho watoto na vijana watapata elimu ya michezo" amesema Mh. Shonza.
Aidha Shonza amewataka viongozi wa Halmashauri ya Pangani na Wilaya zingine Mkoani humo kutenga fedha kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja.
"Viongozi wa Halmashauri tengeni fedha za kukarabati viwanja vya michezo katika maeneo yenu ili vijana wapate maeneo mazuri yakufanyia shughuli za michezo na hii itawajenga zaidi kiushindani" ameongeza.
No comments:
Post a Comment