Sanchi afunguka kuvaa nusu utupu kumempa mchumba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 7 January 2018

Sanchi afunguka kuvaa nusu utupu kumempa mchumba

MWANAMITINDO Jane Rimoy ‘Sanchi’ ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uvaaji wake wanguo zinazo muonesha akiwa nusu utupu, amefunguka kuwa, pamoja na kwamba watu wanampiga vijembe na kumuona mwanamke asiyefaa kutokana na uvaaji wake huo, lakini ukweli ni kwamba ndiyo umempa mchumba.

Sanchi alizungumza kuwa, anashangaa watu wanavyombeza wakati yeye ni mwanamitindo hivyo hakuna cha ajabu katika vazi lake lolote nandiyomaana mwanaume ambaye anataka kumchumbia, amemchagua na kujua wazi anafaa kuwa mke. “Watu hawaelewi maana ya uanamitindo.
Ndiyo maana wanaweza kukusema bila kujua. Kama ingekuwani kinyume cha maadili, basi hata mchumba asingejitokeza,” alisema Sanchi.

No comments:

Post a Comment