Lazima mtu apigwe uwanja wa Amaani leo - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 7 January 2018

Lazima mtu apigwe uwanja wa Amaani leo

SINGIDA United imeshafuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi ikiwa na alama 12 ikiongoza kundi lao, lakini leo Jumatatu watakamilishaa mechi ya kundi hilo kucheza dhidi ya Yanga, huku kocha wake, Hans Pluijm akitamba kuinyoosha.

Hata hivyo, wapinzani wao wamejibu mapigo kwamba Singida isijidanganye kwani wangependa kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Yanga usiku wa jana ilikuwa ikivaana na Zimamoto na kama imepata ushindi ina maana watalingana pointi na Singida na kutofautiana uwiano wa mabao kabla ya kuvaana usiku wa leo kukamilisha ratiba na kujua nani ataongoza kundi lao.

Kocha wa Singida, Hans Pluijm aliyewahi kukinoa Yanga alisema mechi hiyo ni ya kawaida kwake lakini atajipanga kuhakikisha anapata matokeo ya ushindi.

Pluijm alisema ameiona Yanga na anaijua vizuri na hata kama ameshafuzu katika hatua ya nusu fainali anaichukulia mechi kwa muhimu.

“Mechi nzuri japo tumechoka lakini tumejipanga kushinda,” alisema Pluijm.

No comments:

Post a Comment