Mfungwa afufuka ajikuta yupo mochwari - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 9 January 2018

Mfungwa afufuka ajikuta yupo mochwari

Mfungwa mmoja amezinduka na kujikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti baada ya madaktari watatu kuthibitisha kuwa alikuwa amefariki, vyombo vya habari Uhispania vimetoa taarifa hiyo.

Gonzalo Montoya Jiménez alikuwa ni mfungwa katika gereza Asturias na alizinduka saa chache kabla ya kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kugundua chanzo cha kifo chake.

Gonzalo yupoa chini ya uangalizi wa madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Oviedo. Mmoja wa ndugu zake ameliambia gazeti la La Voz de Asturias kwamba Gonzalo “alikuwa amewekewa alama ya kufanyiwa upasuaji, tayari kupasuliwa”.

Wataalamu wamesema hali hiyo inaitwa ‘catalepsy’ ni hali ambayo ishara muhimu za uhai hufifia kwenye mwili wa binadamu kiasi cha kutoweza kutambulika kama yupo hai.

No comments:

Post a Comment