Simba SC, Mbeya City zavuna Mil 74 - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday 6 November 2017

Simba SC, Mbeya City zavuna Mil 74

Mechi ya Mbeya City dhidi ya Simba iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya mwishoni mwa wiki imeiingiza Sh74.6 milioni.

Mapato hayo yameshindwa kuvunja rekodi iliyowekwa kwenye uwanja huo wakati Mbeya City ilipocheza na Simba kwa mara kwanza Sh 105milioni katika msimu wa 2012-13.

Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mbeya, (Mrefa), Haroub Selemani alisema katika mgawao wa mapato hayo, City imejipata kitita cha Sh23.663 milioni na Simba walipata Sh11.831 milioni.

Selemani alisema kiasi kilichobaki kilikwenda kwa wamiliki wa uwanja Sh8.873 milioni, kodi Sh11.381 milioni, Shirikikisho la Soka Tanzania (TFF) sh2.957 milioni, Bodi ya ligi (TPLB) Sh5.324 milioni, Baraza la Michezo Tanzania (BMT) sh591.578, Chama cha Soka Mkoa (Mrefa) Sh1.774 milioni na gharama za mchezo Sh4.141 milioni.

“Hii kwa kweli imevunja rekodi ukiachana na mechi ya kwanza kabisa ya Mbeya City ilipochezwa hapa baada ya kupanda daraja. Lakini miaka mingine yote hatujawahi zidisha Sh40 milioni,” alisema Selemani.

"Hata hivyo uwanja wetu haupo katika mazingira mazuri sana tungeweza kupata zaidi ya kiasi hicho. Kwa mfano hili eneo la jukwaa kuu tungeweka uzio ambao linakuwa na kiingilio chake na upande mwingine unakua na kiingilio chake na mageti ya kuingilia yanakuwa tofauti," alisisitiza kiongozi huyo wa MRFA

No comments:

Post a Comment