Shomary aja na mkakati huu klabu ya Simba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Shomary aja na mkakati huu klabu ya Simba

KIUNGO wa Simba, Ally Shomary amesema tathmini ya kazi aliyofanya katika mechi tisa, amebaini anahitaji kuongeza nguvu zaidi ili aweze kupata namba ya kudumu.

 Alitaja mambo anayoyazingatia timu yake inapocheza kuwa anapopata nafasi anaangalia muda aliocheza na kutathimini mchango wake ulivyoisaidia timu na hata akitokea benchi pia anajifunza kwa nini anabadili nafasi ya mchezaji anayetoka.

 "Nimeishajifunza kitu katika mechi tulizocheza, naamini kitanipa hatua mbele kwa mechi zijazo,najua nyota waliopo ndani ya kikosi chetu wana ushindani mkali wa kushikiria namba pindi wanapopata nafasi,"alisema. "Kocha hawezi kukuacha endapo ukiwa na huduma anayoona italeta matunda kwa kila mchezo ndiyo maana nasema najituma kwa kadri ninavyoweza ili kufikia malengo ya kupata namna ya kudumu,"alisema.

No comments:

Post a Comment