Jennifer Kyaka ‘Odama’.
MSANII wa filamu mwenye uwezo mkubwa awapo mbele ya kamera, Jennifer Kyaka ‘Odama’, amepangua ishu ya kuonekana anajitenga na wasanii wenzake ambapo kila mara anaonekanakivyakevyake tofauti na wasanii wengine.
Odama ameiambia Kilinge kuwa yeye haamini kama anajitenga lakini kuna wakati ni lazima afanye kazi zake, kwa maana siyo rahisi kila muda kukutana kama ilivyozoeleka huko nyuma, kwani maisha yamebadilika sana, ni lazi m a wakutane kwenye kitu maalum.
“Unajua watu hawaelewi tu, mtu anapobadili mfumo kidogo wanasema ameanza kujitenga, kitu ambacho siyo kweli, wakati wa sasa hakuna sababu ya kukutana kila mara, maana kuna vitu vingine vinakuwa haviendi kabisa tukiwa tunajikusanya " alisema Odama
No comments:
Post a Comment