Omog anawa mikono kwa Tshishimbi - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 30 October 2017

Omog anawa mikono kwa Tshishimbi

Kocha wa Simba, Joseph Omog ameukubali uwezo wa kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi na kudai kuwa alikuwa kikwazo kikubwa kwao kupata ushindi juzi Jumamosi walipotoka sare ya 1-1 na watani zao hao.

Omog ambaye amewahi kushinda kombe la Shirikisho Afrika ambalo Simba itashiriki mwakani, alikwenda mbali na kusema kuwa, Tshishimbi ni aina ya viungo ambao timu inahitaji kuwa nao hasa inaposhiriki michuano ya Kimataifa.

Tshishimbi amesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland ambayo ilifika hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho mapema mwaka huu. Mechi ya juzi Jumamosi ilikuwa ya pili kwake dhidi ya Simba baada ya kucheza ile ya Ngao ya Jamii pia.

"Ni mchezaji mzuri sana, anaijua kazi yake vizuri. Alikuwa kikwazo kikubwa sana kwetu," alisema Omog alipoanza kumueleza Tshishimbi ambaye ni mzaliwa wa DR Congo.

No comments:

Post a Comment