SIMON Msuva amewaambia Yanga kwamba ushindi mkubwa wa timu hiyo kwenye misimu ya hivi karibuni, ulikuwa unatokea kwenye mashambulizi ya pembeni, hivyo waliobaki wanapaswa kujiamini zaidi.
Msuva ambaye Yanga imemuuza kwenda klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, ameongeza kuwa kukosekana kwake katika kikosi hicho kumepunguza nguvu kwa kiasi fulani, lakini anamini bado ni mapema kulaumiana.
“Linaweza kuwa tatizo kama Yanga isipopata mchezaji anayeweza kucheza vizuri zaidi akitokea pembeni kwani mara nyingi nafasi za kufunga tangu nilipokuwa Yanga huwa zinatokea pembeni,” alisema Msuva na kuongezea kuwa wapo wachezaji ambao wana uwezo wa kucheza nafasi yake, lakini wanatakiwa kujiamini na kujitambua kama wanaweza.
Tambwe aenda kwao
Taarifa zilizothibitishwa na benchi la ufundi la Yanga ni kwamba mastraika Amissi Tambwe na mwenzake Obrey Chirwa, kila mmoja ameomba ruhusa ya kurudi kwao mara moja na watarejea kabla ya mechi na Kagera.
Chirwa ambaye mashabiki wengi wanamtaja kama raia wa Zambia, ni Mmalawi na ameondoka akilalamika kuwa na maumivu ya paja huku Tambwe akirudi kwao Burundi.
No comments:
Post a Comment