Wolper arudisha mapenzi kwa Harmonize - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 20 October 2017

Wolper arudisha mapenzi kwa Harmonize

KATIKA moja ya mahojiano na kituo cha habari, Jackline Wolper amewahi kukiri wazi kuwa huwa hapendi kumkumbuka na kumpa nafasi mtu ambaye alimpenda na wakaachana.

Hali imekuwa tofauti baada ya Wolper kuonekana kama kalainika kwa aliyekuwa mpenzi wake huyo wa zamani, hasa baada ya kuweka video kadhaa zikimuonesha akicheza na kufurahia wimbo mpya wa Harmonize unaoitwa Shulala aliomshirikisha msanii wa Nigeria, Korede Bello.

Katika video hizo ameweka baadhi ya maneno huku akiusifia wimbo akisema uliyemchokoza kaja na hivyo kuonekana ni kama dongo kwa Sarah ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa Harmonize kwa sasa.

“Haka ka nyimbo kazurii sana na video pia ndio usiseme, bwana Raaaaaj umejua kunyoosha, kama bado hujaangalia video ya haka ka wimbo pita kwenye bio ya @Harmonize_tz ,” aliandika.

No comments:

Post a Comment