Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema hitilafu imetokea katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kipawa jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Tanesco iliyotolewa leo Jumatatu Oktoba 30,2017 na ofisi ya uhusiano makao makuu imesema hitilafu imetokea saa 11:51 asubuhi.
Kutokana na hitilafu hiyo, Tanesco imesema Gongo la Mboto, Air Port, Chang'ombe na baadhi ya maeneo ya Tabata na Buguruni hayana umeme.
Shirika hilo limesema mafundi wanaendelea na jitihada za kurekebisha hitilafu hiyo na kwa haraka.
Kutokana na hilo, Tanesco imewaomba radhi wateja kwa usumbufu unaojitokeza.
Pia, limetoa tahadhari kwa wananchi kutoshika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.
No comments:
Post a Comment