Dyna Nyange na Diamond wamemaliza bifu lao kiutuuzima - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 12 October 2017

Dyna Nyange na Diamond wamemaliza bifu lao kiutuuzima

Mwimbaji Dayna Nyange ambaye aliwahi kuingia katika bifu na Diamond Platnumz wameweka sawa tofauti zao, baada ya kumtuhumu kuwa alimuibia wimbo wa My Number One, njama ambayo anasema walifanya pamoja na Sheddy Clever ambaye alikuwa produza.

Hivi karibuni kupitia kurasa yake ya Instagram aliposti video ambayo iliwaonesha wakiwa pamoja huku wakifurahia kwa kucheza muziki na kuimba hali iliyoonesha kuwa hali kwa upande wao ipo freshi siyo kama mwanzo.

Dayna Nyange amekiri kuwa kwa sasa wamemaliza tofauti zao na maisha yanaendelea kama kawaida.

“Kuna sehemu mnafikia kwenye maisha inabidi tu mambo Fulani muyamalize,kwahiyo tulikutana wakati kwanza mimi nilikuwa naenda kuomba viza ndipo mara ya kwanza tulianza kuongea,”

“Na kwenye tuzo pia tulikuwa pamoja na hata alipochukua tuzo nilifurahi sana, kiufupi sasa tupo fresh na maisha yanaendelea,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment