Simba SC kukipiga na wababe wa Dodoma Jumatano hii. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 3 October 2017

Simba SC kukipiga na wababe wa Dodoma Jumatano hii.

Baada ya kuifunga Stand United ‘Chama la Wana’ na kushika usukani wa msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, Simba SC hapo kesho siku ya Jumatano Oktoba 4, watashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma FC Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kocha mkuu wa timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi, Joseph Omog atatumia nafasi hiyo muhimu kukitathimini kikosi chake katika kipindi hiki ambacho VPL imesimama kupisha mchezo wa kalenda ya FIFA.

Omog atavaana na kocha mwenye historia na Simba na mwenyemaneno mengi katika mchezo wa soka hapa nchini Jamhuri Kiwhelo Julio ‘Pereira’ ambaye amakinoa kikosi cha Dodoma FC ambacho kinashiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara ‘FDL’.

Katika mchezo uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku mchezaji, Shiza Ramadhan Kichuya na Laudit Mavugo wakipachika magoli hayo na kuifanya kukwea kileleni kwa pointi 11.

No comments:

Post a Comment