Nsajigwa amekiri Yanga kuwa na tatizo la ukame wa mabao. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday 9 October 2017

Nsajigwa amekiri Yanga kuwa na tatizo la ukame wa mabao.



Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa 'Fuso' amekiri kuna tatizo ndani ya timu hiyo hasa eneo la ushambulaiji na wanaendelea kupambana nalo ili kuhakikisha mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar mabao yanapatikana.

Yanga ilitoka suluhu na KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Kutokana na suluhu hiyo mashabiki wengi wa Yanga wameonekana kukosoa uchezaji wa kikosi hicho huku wakimlamu kocha George Lwandamina kuwa ameshindwa kazi.

Nsajigwa alisema timu inacheza vizuri, lakini tatizo kubwa lipo kwenye ufungaji wa mabao na wanaendelea kulitafutia ufumbuzi jambo hilo ili kuhakikisha wanashinda mabao mengi michezo inayofuata.

"Kuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji, mabao yanakataa, timu haifungi ni jambo linalotuumiza na tunaendelea kuhangaika nalo ili kuhakikisha tunarejea katika ubora wetu.

"Wachezaji wengi wanaocheza eneo hilo ni wagonjwa na wengine hawako fiti pia ukiangalia hata katika mchezo huo tumetumie baadhi ya wachezaji ambao hawachezi mara kwa mara."alisema Nsajigwa.

Yanga itashuka tena uwanjani Jumamosi hii kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba.

No comments:

Post a Comment