Kocha yanga azichapa kavukavu - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 29 October 2017

Kocha yanga azichapa kavukavu

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa aliamua kuzikunja na kutupiana makonde kidogo na makomandoo wa Simba waliomzuia kuingia kwenye chumba cha mikutano baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Haikuweza kufahamika mara moja kama makomandoo hao hawakujua kama Nsajigwa alikuwa akienda huko ama walifanya hivyo kumzingua kocha huyo kwa kumsukuma na yeye kuhamaki kama ya kurushiana ngumi na askari polisi kuingilia kati kuwaamulia na mambo kumalizika.

Katika mchezo huo wa watani wa jadi ulishudia Yanga ikililazimisha sare baada ya Obrey Chirwa kuisawazishia dakika 60, akifuta lile la Shiza Kichuya aliloifungia Simba dakika 57 ya mchezo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha wa Simba, Joseph Omog wa Simba alisema 'Mechi ilikuwa ngumu kama ilivyo kawaida, lakini malengo yetu yalikuwa kupata pointi tatu na tulistahili, ila niwapongeze Yanga kwani ni timu nzuri na wachezaji wake wanacheza vizuri na tunajipanga kwa mechi zijazo."

Naye Nsajigwa alisema kama wachezaji wake wangekuwa makini jana wangetoka na ushindi mbele ya Simba kwani walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia.

"Katika mchezo huu tuliwakosa wachezaji wetu watatu (Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko), lakini tunashukuru kupata hata hiyo pointi moja," alisema nahodha huyio wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.

Simba ilianza kwa kasi na kufanya majaribio mawili ya haraka katika dakika ya kwanza tu kupitia kwa Laudit Mavugo lakini mashuti yake yalikwenda nje kidogo ya lango.

Mpira ulitulia na kucheza zaidi katikati ambapo Simba ilijaribu kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa lakini hadi dakika 20 za kipindi cha kwanza zinamalizika ni Haruna Niyonzima pekee aliyeweza kufanya jaribio moja ambalo hata hivyo halikuwa na madhara.

Uwezo mkubwa wa viungo hasa Papy Kabamba Tshishimbi wa Yanga na James Kotei wa Simba ulisababisha timu zote zishindwe kufanya mashambulizi ya maana kwani katika dakika 20 za mwanzo hakukuwa na shuti hata moja lililolenga lango.

Yanga ilituliza akili na kuanza kujenga mashambulizi kupitia pembeni kwa Geofrey Mwashiuya na Pius Buswita na yalizaa matunda dakika ya 23 ambapo kipa wa Simba alitumia jitihada binafsi kuokoa shuti kali ya Mwashiuya.

Dakika ya 24 hadi 30 Yanga iligeuka mbogo na kulisakama lango la Simba lakini Manula alikuwa makini na kupangua mashuti mawili ya Mwashiuya na Tshishimbi ambaye ndiye alikuwa nyota wa mchezo kwa Yanga.

Mpira ulipooza na kuwa na ufundi mwingi katika dakika 15 za mwisho

No comments:

Post a Comment