Diamond kutuletea nyimbo yake nyingine na Rick Ross - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 12 October 2017

Diamond kutuletea nyimbo yake nyingine na Rick Ross

Diamond Platnumz ameonekana akiwa yupo kwenye maandalizi ya kuandaa video mpya na mkali Rick Ross mjini Miami, Marekani.

Kuna baadhi ya video zimekuwa zikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikimuonesha Diamond akiwa na Rick Ross huku wakiwa wamezungukwa na kamera mbalimbali na watu kadhaa wakiendelea na kazi.

Tayari muongozaji Mr Moe Musa kwa mara nyingine, ndiye alithibitika anaandaa mchongo huo ambao ulianza kutajwa na Diamond tangu muda na hivi karibuni ambavyo Diamond amekuwa balozi wa kinywaji cha Belaire ambacho ndicho pia Rick Ross ni balozi hivyo kolabo yao imekuwa rahisi zaidi.

Upande wa pili wa maisha ya mkali huyo wa Bongo Fleva, Zari alishathibitisha kuwa uhusiano wao upo vyema na walichoamua kwa sasa ni kutokufanya yawe ya wazi kama zamani.

Upande wa pili kwa Hamissa Mobetto, nae ameendelea kupambana na hali yake ambapo ameenda kumshtaki Diamond Platnumz kuhusu suala la malezi ya mtoto wao ambapo taarifa za chini chini zinasema kuwa Diamond amekatisha huduma zote za mtoto.

Yote hayo yakiendelea, Diamond kwa sasa kuna uwezekano wa kumaliza mwaka kwa mafanikio mazuri kimuziki hasa baada ya kunyakua tena tuzo ya Afrimma kama Mwanamuziki bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki na singo yake ya Hallelujah inayoendelea kukimbiza.

No comments:

Post a Comment