KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amefichua kuwa bado timu hiyo inahitaji mchango wa aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji ambaye alijiuzulu mwezi Mei mwaka huu.
Sanga ambaye kwa sasa ndiye kiongozi wa juu wa Yanga, alisema kwa sasa ni ngumu kwa klabu hiyo kumpata mtu aina ya Manji ambaye alikuwa haoni shida kutoa fedha zake za mfukoni ili kusaidia shughuli za klabu.
“Katika hali ya kawaida sasa ni ngumu kumpata mtu aina ya (Yusuf) Manji, alikuwa akijitolea sana kwaajili ya timu, siyo mchoyo wala mbinafsi,” alisema Sanga ambaye anawania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu.
“Kama tunahitaji kushindana zaidi uwanjani tunamhitaji Manji. Lakini kila mtu ana maoni yake, wanaweza kusema tunafanya kazi kubwa kwa sasa hadi kuanza kukarabati uwanja ila bado Manji anabaki kuwa pengo kubwa ndani ya timu.
“Siwezi kusema kama atarudi ama la kwa kuwa ndiyo kwanza ametoka kwenye matatizo na bado hajakaa vizuri, ninadhani hilo ni yeye mwenyewe kuamua kurudi ama la,” alisema Sanga.
Uwekezaji Simba
Katika hatua nyingine, Sanga alisema uwekezaji unaofanywa Simba kwa sasa hauwezi kuwasumbua sana kwani ni kama wanaiuza timu yao kwa watu wachache tofauti na mfumo waliotaka kuufuata wao Yanga.
“Hofu yangu ni kwamba timu yao itakuwa imekwenda kwenye mikono ya watu wachache, ni tofauti na Manji alipotaka tuikodi timu kwake. Yetu ilikuwa ni ya muda lakini kwao ni ya moja kwa moja,” alisema Sanga.
“Sisi pia Katiba yetu inaturuhusu mfumo wa Kampuni lakini Wanachama watamiliki asilimia 51, hii ni nzuri pia kuliko ya Simba.”
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment