Msuva,Samagol,Banda wakinukisha - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 13 October 2017

Msuva,Samagol,Banda wakinukisha

Nyota wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ataipeperusha bendera katika klabu zao katika mechi mbalimbali wikiendi hii.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ataiongoza KRC Genk kesho kuivaa Royal Excel Mouscron katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji kwenye uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena .

Rekodi zinaipa timu ya Samatta asilimia 74 kwa katika mechi saba walizocheza dhidi ya wapinzani wao hao wameshinda mechi tano na kutoka sare mmoja na kufungwa mmoja.

Ukiacha Samatta naye beki Abdi Banda anayechezea Baroka inayoongoza Ligi Kuu Afrika Kusini anategemea kuingoza timu yake hiyo kwenye idara ya ulinzi itakapocheza na Golden Arrows, Oktoba 18.

“Ushindi utatufanya kuendelea kujiwekea mazingira ya kupigania ubingwa japo ni mapema ila michezo hii ya mwanzoni  huwa na mchango mkubwa kwenye mbio za ubingwa,” alisema Banda.

Saimon Msuva aliifungia Taifa Stars bao la kusawazisha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi Oktoba, 7 ameendeleza makali yake katika klabu yake Difaa Hassani El Jadidi akifunga bao moja katika mchezo walionyukwa kwa mabao 2-1.

“Kombe la  Moroccan Throne Cup, huo ni mchezo wa kwanza kucheza nilivyorudu kutoka Tanzania, nimekuwa sehemu ya timu kupata bao la ugenini hilo ni jambo la kujivunia, tupo katika hatua nzuri ya kusonga mbele.

 “Kuhusu kufunga huwa kunakuja ila muhimu zaidi ni kuisaidia timu kupata matokeo mazuri, kufunga alafu timu haishindi na kutokufunga alafu ukatengeneza nafasi ya bao na timu ikashinda kipi bora?.

“Napenda sana kufunga tangu nikiwa Yanga, lakini kipaumbele cha kwanza ni kuisaidia timu, ujue hata nisipofunga huwa hali yangu ya kujiamini uwanjani haipungui kabisa,” alisema Msuva ambaye mchezo wao ujao wa Ligi nchini humo watacheza na Moghreb Tétouan.

Mshambuliaji Elias Maguri na Salum Shebe wanaocheza Ligi Kuu Oman, watazitumikia timu zao leo kwenye viwanja tofauti, Maguri atakiongoza kikosi chake cha Dhofar dhidi ya Al Suwaiq ugenini.

Kiungo Shebe naye ataipigania timu yake ya Al-Mudhaibi ili kuinasua kwenye mkia wa Ligi hiyo itakapocheza na nyumbani na Al Salam.

Kiungo mwingine anayeichezea FC Chiasso ya Ligi daraja la kwanza Uswizi, Said Mhando timu yake itakua na kibarua cha kutafuta matokeo mbele ya Neuchatel Xamax, Oktoba 15.

Winga wa Kitanzania Michael Lema wa Sturm Graz ya Austria, huenda akapata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo dhidi ya Austria Wien, Oktoba 15.

FC Tenerife ya Farid Mussa na yenyewe itakuwa na mchezo wa Ligi daraja la kwanza Hispania leo dhidi ya Numancia, Farid anaendelea kupigani nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Watanzania wanaocheza Ligi Kuu Kenya, Hamisi Abdalla  wa Sony Sugar na Abdul Hilal wa Tusker wanategemewa kuziongoza timu zao kupigania matokeo ya ushindi kwenye Ligi hiyo.

Hamisi aliyepata majeraha kwenye ule mchezo wa kirafiki uliopita wakati akiitumia Taifa Stars dakika ya 10 huenda akawa sehemu ya kikosi cha Sony Sugar kitakachocheza na Nzoia Sugar Oktoba 15 kama atakuwa fiti kwa asilimia zote.

Naye Abdul yupo fiti kuisaidia timu yake ya Tusker kwenye mchezo watakao kuwa nyumbani dhidi ya Muhoroni Youth.

No comments:

Post a Comment