Aguero baada ya kunusulika kifo sasa amepata janga lingine. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 2 October 2017

Aguero baada ya kunusulika kifo sasa amepata janga lingine.


Ikiwa ni siku tano zimepita tangu mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero kupata ajali mbaya ya gari nchini Uholanzi iliyompelekea kuvunjika mbavu, mkali huyo wa kucheka na nyavu amepata mshituko mwingine kwa kuachwa na mchumba wake wa miaka minne.

Mchumba wake huyo ajulikanaye kwa jina la Karina Tejeda (31) ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Argentina amechukua uamuzi huo akidai kuwa Aguero alikuwa msiri kwenye mahusiano yao.

Mrembo huyo kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Telefe cha nchini Hispania amekiri wazi kuwa mawasiliano yake na mshambuliaji huyo yalikuwa ya kusua sua na mara nyingi huwa wanakutana anaporudi kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa.

Karina anayefahamika kwa jina la The Princes’ nchini Argentina amesema amekuwa akijihisi mwenye kasoro kwani hata anapoweka posti kwenye mitandao ya kijamii Aguero amekuwa hajibu na hata akimtumia meseji zinachelewa kujibiwa.

“Inawezekana sio mzuri, najiona kama si kitu japo tumetoka mbali tumezoeana ila ni vizuri tukaendelea kuishi kwa furaha kama tulivyokutana, “amesema Karina.
Moja ya Tweet zake alizoandika Karina zikimlenga Aguero.

Hata hivyo, mrembo huyo ameongeza kuwa ameshawahi kugombana na Aguero kwa tabia za kwenda klabu na marafiki zake bila kumtaarifu.

Uchumba wa Aguero na Karina uliwavutia Waargentina wengi na ulitajwa kuwa uchumba wenye mvuto nchini humo.

No comments:

Post a Comment