Kiungo Papy Tshishimbi ataukosa mchezo ujao wakati Yanga itakapoivaa Mtibwa Sugar.
Yanga itaivaa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi ijayo.
Ataukosa mchezo huo baada ya kulambwa kadi ya njano ambayo inakuwa ya tatu katika mechi nne.
Hii inamfanya Mkongo huyo kurejea jukwaani wakati Yanga ikipambana.
No comments:
Post a Comment